Friday, July 22, 2016

MICHEZO Dalili nyingine ya kuwa Paul Pogba atatua Man United msimu huu



Klabu ya Manchester United inayofundishwa na kocha mreno kwa sasa Jose Mourinhoimerudi kwenye headlines baada ya July 21 kutoa namba za jezi watakazovaa wachezaji wake kwa msimu wa 2016/2017, Man United wametangaza namba hizo za jezi na kuiacha namba ambayo inaaminika kuwa katengewa Paul Pogba.
Man United ambayo usiku wa July 20 iliripotiwa na na The Sun kuwa imekubaliana naJuventus ya Italia kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba kwa dau la pound milioni 105, inatajwa kuacha jezi namba 6 wazi, kitu ambacho kinatsirika kuwa ni namba ya jezi ambayo kawekewa Paul Pogba.
Manchester-United-Squad-Numbers-1024x1024
Wachezaji wapya wa Man United wote washapewa namba za jezi kama Zlatan Ibrahimovic atavaa jezi namba 9 iliyokuwa inavaliwa na Anthony MartialEric Baillyatavaa jezi namba 3 na Henrikh Mkhitaryan atavaa jezi namba 22. Pogba wakati anaondoka Man United 2012 alikuwa akivaa jezi namba 42.





Man United yaweka hadharani namba za jezi za wachezaji wao, namba 6 ni ya Pogba

Timu ya Manchester United imeweka hadharani namba ya jezi za wachezaji wao watakazozitumia kwa msimu wa mwaka 2016/2017.
wit-the-kids

Mshambuliaji mpya aliyesajiliwa hivi karibuni kwa uhamisho huru, Zlatan Ibrahimovic amekabidhiwa jezi yenye namba aliyozoea kuvaa muda mrefu yenye namba 9 iliyokuwa ikivaliwa na Antonio Martial klabuni hapo na sasa mchezaji huyo atakuwa anavaa jezi yenye namba 11 iliyokuwa ikivaliwa na nguli wa timu hiyo Giggs na kinda Januzaj.
Aidha kwenye orodha iliyotolewa na timu hiyo inaonyesha kuwa jezi namba 6 haijapata mvaaji huku kukiwa na taarifa kuwa imewekwa maalumu kwa kiungo Paul Pogba anayetarajiwa kutua klabuni hapo kwa uhamisho utakaoweka rekodi ya dunia wa paundi milioni 100.


Julen Lopetegui atangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Spain


Kocha wa zamani wa FC Porto, Julen Lopetegui ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Spain akirithi mikoba ya Kocha Vicente Del Bosque aliyeondoka baada ya kufanya vibaya katika michuano ya Euro 2016 France.

2CDC2EB400000578-0-image-a-20_1443449279840

Julen,49, ambaye aliwahi kuwa mchezaji alikuwa kipa, amewahi pia kufundisha timu ya Taifa ya Spain chini ya miaka 19 na Chini ya miaka 21.


Bill Nas akana kufanya biashara haramu

Msanii wa Hip Hop Bongo, Bill Nas amekuwa akihusishwa na biashara haramu kutokana na kushoot video kali na za gharama tofauti na hela aliyoipata mpaka sasa kwenye muziki wake.
Billnass

Rapper huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, “Wasanii wengi hatupendi kuwekeza kwenye vitu vyetu.”
“Mimi nasoma biashara na elimu ya kwanza unapopata hela kwanza wekeza, unasave halafu kile kinachobakia unaweza uka-spend. Kwahiyo mimi bado nawekeza kwenye muziki wangu bado sijaanza kuspend kwa sababu naipenda kazi yangu,” ameongeza.
“Hata kwenda kushoot video Afrika Kusini nina risk sana kwa sababu siyo kama hela hizo zinarudi.”
Mpaka sasa Bill Nas ameshaachia nyimbo tatu huku wimbo wake wa ‘Chafu Pozi’ ukizidi kufanya vizuri kwenye radio na TV.


Zuio la Mikutano ya Kisiasa ni Kumyima Mwanchi Uhuru wa Haki ya Kujumuika- Kijo Bisimba.



Serikali imetakiwa kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ambazo zimeonekana kuwa kandamizi ikiwepo ile sheria za vyombo vya habari ambazo zinakandamiza uhuru wa vyombo vya habari pamoja na waandishi wenyewe.

Akitoa ripoti ya nusu mwaka mbele ya wanahabari kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa vyombo vya habari havifanyi kazi kwa uhuru kwani zipo sheria ambazo bado ni kandamizi.

”Vyombo vya habari bado havina uhuru kwani sheria kandamizi bado zinatumika mfano, gazeti la mawio kufungiwa na kutakiwa kutoandika nakala zake hata kwenye mitandao bila sababu maalumu”.Ilielezwa katika ripoti ya kituo hicho

Aidha ripoti hiyo ya miezi sita imesema kuwa wananchi bado wananyimwa haki zao za msingi  ikiwa ni pamoja na  kunyimwa haki ya habari kwasababu  serikali imeamua kutorusha matangazo ya bunge kwa sababu mbalimbali ambazo zinakinzana.

Katika ripoti hiyo pia imegusa haki za kujumuika ambapo kituo hicho kimesema matamko ya jeshi la polisi hasa katika kuzuia mikutano ya vyama imeonekana  kupendelea chama tawala huku vyama vya upinzani  vikiwa vinakandamizwa.

”Mfano mkutano wa Chadema shinyanga ulipewa vibali vyote lakini baadae ukaja kutawanyishwa kwa kutumia nguvu mpaka mabomu, aidha ACT walikuwa na kongamano la kuchambua bajeti lakini jeshi la polisi walizuia lakini wakati huo huo CCM walikubaliwa kufanya mkusanyiko” Ilieleza semu ya ripoti ya Kijo Bisimba.

Pamoja na hayo ripoti hiyo imetoa mapendekezo kwa Serikali  ikiwa kuboresha sheria hizo kandamizi kwa wananchi pamoja na kuachia vyombo vya habari kufanya kazi zake pasipo kuingiliwa sambamba na Vyama vya siasa kupewa haki sawa.

Maalim Seif kutinga Mahakama ya ICC leo Kuwashitaki Viongozi wa Serikali



Chama cha Wananchi (CUF) kimesema katibu wake mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad leo atakwenda katika Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) kuwashtaki viongozi wa Serikali kwa madai walitumia mamlaka yao vibaya wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kisha kuwatesa, kuwakamata na kuwapiga wafuasi wa chama hicho bila makosa.

Chama hicho kikuu cha upinzani Zanzibar, kimesema taratibu zote za kufungua mashtaka hayo zimeshakamilika, ikiwa ni pamoja na kuweka wakili.

Mei 22 mwaka huu, chama hicho kilizindua ripoti yake ya uvunjwaji wa haki za binadamu Zanzibar wakati wa uchaguzi huo na kutangaza azma yake ya kwenda ICC kuwashtaki Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema mpango huo umekamilika na Maalim Seif ambaye yuko nje ya nchi kwa ziara ya kueleza alichodai ‘figisufigisu’ zilizotokea katika uchaguzi mkuu, ataweka wazi kila kitu kilichotokea na jinsi ukiukwaji wa demokrasia ulivyoshika kasi nchini.

Mazrui alimtuhumu IGP Mangu kuwa anatumiwa na CCM kuwakamata viongozi wa CUF ili wasitimize azma yao ya kueleza ukweli wa yaliyotokea katika uchaguzi, huku akimtaka afute azma yake ya kumkamata Maalim Seif kwa maelezo kuwa “ataitumbukiza Zanzibar kwenye machafuko”.

Siku tano zilizopita, IGP Mangu wakati akihojiwa na Azam TV alisema Jeshi la Polisi wakati wowote litamburuza mahakamani Maalim Seif kwa kuhamasisha uchochezi Zanzibar. Iwapo CUF itatekeleza azima hiyo, itakuwa tukio la kwanza kwa Tanzania kupeleka viongozi wake kwenye mahakama hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na naibu wake, William Ruto wameshafikishwa huko, lakini kesi dhidi yao zilikosa nguvu na kuondolewa.

Katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Salim Jecha Salim alifuta matokeo ya rais, wawakilishi na madiwani Oktoba 28, mwaka jana siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa mbio za urais.

CUF ilidai kuwa ilishinda uchaguzi huo na Jecha alipotangaza uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu, chama hicho kilijitoa na hivyo CCM kushinda viti vyote.

Mazrui ambaye aliambatana na viongozi wengine wa chama hicho alisema: “Mpango wa kuishawishi dunia kuwachukulia hatua wahusika wote wa ukiukwaji wa haki za binadamu na uvunjwaji wa demokrasia uko palepale, hautasitishwa kwa vitisho vyovyote.

 “Lengo ni kuhakikisha unyama dhidi ya raia wasio na hatia unakomeshwa na uzingatiwaji wa sheria za nchi unatamalaki. Tunawaambia polisi kuwa tumechoshwa na figisufigisu maana zitazaa timbwiri.”

Mazrui alisema wanaotaka kuzuia mpango wa CUF kueleza ukweli na kwenda ICC, wanaandaa utaratibu wa kumkamata Maalim Seif aliyedai; “Ni kipenzi cha Wazanzibari”, akisisitiza kuwa jambo hilo ni hatari kwa sababu litaivuruga Zanzibar.

Akifafanua zaidi kile alichokiita mikakati ya CCM kupitia kwa IGP Mangu kuficha ukweli, Mazrui alidai kuwa polisi wamekuwa wakiwakamata wanachama wa CUF mara kwa mara.

"Niongeavyo hapa wanachama zaidi ya 400 wa CUF wamekamatwa na wengine wapo nje wa dhamana,” alisema.

Alisema ni jambo la ajabu kuona IGP Mangu akishindwa kutoa kauli yoyote baada ya Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DDCI), Salum Msangi kuwatishia mawakili kuwatetea wananchi wanaokamatwa kwa tuhuma  mbalimbali.

Alisema viongozi wa CUF hawatatishwa wala kunyamazishwa katika kudai haki ya ushindi wa Wazanzibari kutokana na uamuzi wao wa uchaguzi mkuu.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Shaweji Mketto alisema endapo IGP Mangu ataendelea kuwatisha viongozi wa CUF, watajipanga kwenda kumtembelea ofisini kwake.

IGP Mangu ajibu
Alipoulizwa kuhusu kauli za CUF, IGP Mangu alisema tayari ameshatoa msimamo wa Jeshi la Polisi na walichokifanya viongozi wa chama hicho ni kumjibu tu.

“Ukipendwa sana ukafanya uhalifu tukuache? Tukikutuhumu unafanya makosa tutakukamata hatuwezi kuogopa umaarufu wako,” alisema huku akisisitiza kuwa jalada kuhusu Maalim Seif lipo kwa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka).

“Umesema hao CUF wamesema kuna wanachama wao wamekamatwa, sasa wamekueleza hao wanachama ni kina nani?… kama wamekamatiwa Zanzibar wapo maofisa wa polisi wa mikoa wanaoweza kuzungumzia hilo huko Zanzibar.”

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema: “CCM hatuwezi kujiingiza katika hoja za IGP na CUF tumewaachia wenyewe. Kwa sasa tupo katika maandalizi ya kuhakikisha Rais (John) Magufuli anashinda kwa kishindo kuwa mwenyekiti wa CCM.” Alisema chama hicho hakina sababu ya kutumia Jeshi la Polisi kukandamiza wanachama na viongozi wa CUF.

Nay wa Mitego Afungukia Picha za ‘Pale Kati’ Zilizo Mdhalilisha Mwanamke, Azikana



Msanii Nay wa Mitego ambaye siku za karibuni wimbo wake mpya ‘Pale kati’ umefungiwa na Baraza la sanaa Taifa (BASATA) amefunguka na kusema kuwa suala la watu kusambaza picha kwenye mitandao ya jamii huku zikiwaonyesha wanawake wakiwa hawana nguo kabisa siyo kosa lake yeye kwani hakufanya hicho kitu bali kuna watu walitengeneza hizo picha wakiwa na malengo yao.

Nay wa Mitego amesema hayo katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kudai kuwa kuna watu walikuwa wanatengeneza picha hizo na kuzisambaza ila yeye hajafanya hivyo, na kudai kuwa alishajaribu kuwaripoti watu wengine ambao walikuwa wanafanya mchezo huo.

“Suala la picha za wimbo huo kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii huku zikionyesha wanawake wakiwa nusu uchi si suala langu mimi, maana dunia ya sasa kuna watu wanafanya ‘editing’ ya picha sana, kama mtakumbuka hata kipindi nimetoa ‘Shika adabu yako’watu walinitengeneza sana kwenye picha na kusambaza kwenye mitandao ya jamii, hivyo suala la picha hilo siyo tatizo langu” alisema Nay wa Mitego.

Mbali na hilo Nay wa Mitego amesema kuwa yeye hajaridhishwa na maamuzi ya BASATA kufungia wimbo wake mpya kwa kigezo cha picha kwani walipaswa kusubiri video itoke ndiyo inaeleza vizuri maana ya wimbo wake huo.

“Huwezi kufungia ‘Audio’ kwa sababu ya picha BASATA walitakiwa kusubiri nitoe video kwani video inatoa tafsiri nzuri ya wimbo huo na kama kungekuwa na tatizo kwenye video ndiyo tulipaswa kukaa na hawa walezi wetu katika muziki BASATA ili kuona tunaweza kurekebisha jambo gani katika video” alimalizia Nay wa Mitego

TANZIA: KUNDAMBANDA afariki Dunia



Msanii maarufu wa VICHEKESHO (Komedi) Ndugu. Ismail Issa Makombe a.k.a KUNDAMBANDA, amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo.

Kundambanda alikuwa mgombea ubunge wa CUF na UKAWA kwenye jimbo la Masasi - Mtwara katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Disemba 2015 baada ya ule wa Oktoba kutofanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea wa awali wa UKAWA, Mhe. Emmanuel Makaidi (NLD). Katika uchaguzi huo wa Disemba 2015 Kundambanda alipata kura 14,069 dhidi ya kura 16,597 za (mshindi) Rashid Chua Chua kutoka CCM. Taratibu za mazishi zinafanyikia nyumbani kwao Masasi.  Inna lillah wainailayna rajiun. RIP Kundambanda.

Wednesday, July 20, 2016

Mourinho katoa Top 3 ya wachezaji wake wa muda wote anao wakubali


Kocha wa Man United Jose Mourinho ametoa list ya wachezaji wake watatu wa muda wote na kumuacha Ronaldo baada ya kutoa list hiyo imekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii, Mourinho katika mahojiano na Daily Express ametaja majina ya wachezaji wake watatu wa muda wote.
071916-SOC-real-madrid-cristiano-ronaldo-jose-mourinho.vadapt.664.high_.86

Mourinho amewataja Messi, Pele na Diego Maradona kama ndio wachezaji bora wa muda wote na ameonekana amempotezea mreno mwenzake Cristiano Ronaldo ambaye watu wengi walizani kuwa atakuwemo katika list hiyo ya Mourinho ukilinganisha uwezo wake na utaifa wao “Kwangu mimi binafsi TOP 3 ya wachezaji bora wa muda wote katika historia ni Messi, Pele na Maradona”
Ronaldo amewahi kufundishwa na Mourinho kwa misimu mitatu katika klabu ya Real Madrid na mwaka 2012 alifanikiwa kushinda tuzo ya Ballon d’Or akiwa chini ya Mourinho, kauli hiyo ya Mourinho inaonyesha kuwa na tofauti na Ronaldo lakini wengi hawakutarajia kuona Ronaldo akikosekana katika list hiyo.

Picha: Man United waenda kujifua China

Klabu ya Manchester united wameenda Nchini China katika kujiandaa na msimu mpya.Wakiwa huko China, United watacheza mechi mbili ya kwanza watacheza na klabu ya Borussia Dortmund mjini Shanghai, siku ya ijumaa na kisha jumatatu watacheza na Manchester Man City,jijini Beijing.
article-3697765-366C521800000578-830_636x382

Wameenda jumla ya wachezaji 25 ndio wako kwenye msafara wa timu hiyo wakiwamo nyota wapya Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan pamoja na Chipukizi tisa toka chuo cha soka cha Man United, huku wachezaji wengine walioshiriki michuano ya ulaya wakiachwa kuendelea kupumzika.
Man United wanakwenda katika ziara hiyo wakiwa chini ya kocha wao mpya Jose Mourhino mwenye kibarua cha kurudisha thamani ya timu hiyo.
366B1AE300000578-3697765-The_Manchester_United_squad_have_jetted_off_to_China_as_part_of_-m-1_1468948330507

366B140100000578-3697765-United_s_players_are_ready_for_pre_season_to_go_up_a_gear_in_Chi-a-75_1468943729152

Stereo asimulia alivyomgeuza Ben Pol kutoka kuwa rapper hadi kuwa muimbaji

Hapo zamani za kale, Ben Pol alikuwa rapper.

Stereo

Kama isingekuwa Stereo waliyesoma shule moja, kusingekuwa na hit single kama ‘Moyo Mashine za zingine.
“Ben alikuwa anarap,” Stereo ameiambia Bongo5.
“Sababu mimi nilianza hii michezo siku nyingi anakuja ananiambia ‘Stereo eeh hebu nisikilize’ namsikiliza. Lakini kuna siku alikuwa anaimba kitu nikamuambia ‘Ben rap is not your thing, unarap vizuri, una swag. Kipindi hicho cha akina Hajj Noorah, Chamber Squad ndio ilikuwa crew anayoipenda sana akina marehemu Mangwair (RIP), nikamuambia rap sio kitu chako wewe ni muimbaji,” anasema Stereo.
Anasema alimshauri Ben Pol kuwekeza nguvu zaidi kwenye kuimba na kutojali kama atachelewa kutoka.
“Ben Pol is there so I am proud of him,” ameongeza rapper huyo.


Donald Trump apitishishwa rasmi na chama cha Republican kugombea urais Marekani

Donald Trump hatimaye ateuliwa sasa kuwa mgombea rasmi wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi November mwaka huu. Trump amepata uungwaji mkono na wajumbe kutoka majimbo na wilaya za Marekani katika kura mchujo wa kumpata mgombea wa nafasi hiyo kupitia chama chake cha Republican kupitia mkutano mkuu wa chama chake mjini Cleveland.

160608035103_us_trump_newyork_512x288_reuters_nocredit

Baada ya kuchaguliwa kuwa mgombea urais Donald Trump alitoa shukran zake kupitia mtandao wa twitter,na imetanabahishwa kwamba gavana wa jimbo la Indiana Mike Pence, ndiye mgombea mwenza .Taarifa zaidi zinasema watoto wawili wa Donald Trump wa kiume Donald na pia bintiye Tiffany wanatarajiwa kuhutubia mkutano mkuu wa wanachama wa chama hicho.

Kim Kardashian alipwa shilingi bilioni 1.5 kupiga selfie na mastaa hawa wa Instagram

Wakati ambapo warembo wengi duniani hupiga selfie kuwafurahisha tu followers wao kwenye mitandao ya kijamii, Kim Kardashian anaingiza mkwanja mrefu.
365BE64100000578-3697048-image-m-10_1468917677850

Tovuti ya Page Six imedai kuwa staa huyo mwishoni mwa wiki alilipwa $700,000 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 1.5 kupiga selfie na mastaa Instagram huko Hamptons.
Kardashian, aliyepelekwa huko kwa ndege binafsi, alitokea kwenye Revolve Hamptons House huko Water Mill, LI, Jumamosi iliyopita na kupiga picha na mastaa hao maarufu Instagram kwa saa moja.
Kim pia alikuwa na walinzi 25 kumlinda. Kwa mujibu wa Forbes utajiri wa Kim sasa ni zaidi milioni 51. Hizi ni picha alizopiga na mastaa hao:
365BE63900000578-3693811-image-m-95_1468760519452
365BE6EE00000578-3697048-image-m-8_1468917521903
365BE9C400000578-3697048-image-m-7_1468917508675

365BE9D000000578-3693811-image-a-97_1468760556179

365BE9DB00000578-3693811-Her_own_style_rules_She_teamed_it_with_a_pair_of_thigh_high_deni-m-85_1468760351018

365BE9EF00000578-3693811-image-m-94_1468760493086


365BE9FA00000578-3693811-image-m-92_1468760435120

365BE61800000578-3693811-image-m-80_1468760213563



Hizi Hapa Siri Kumi za Maisha ya Ndoa Kama Unataka Ndoa yako I we na Amani



10 SECRET OF MARRIAGE LIFE

1. *EVERYONE YOU MARRY HAS A WEAKNESS*
Only God has no weakness, Every rose flower has its own thorn

2. *EVERY ONE YOU MARRY HAS A DARK HISTORY*
No one is an angel, avoid digging one's past forgive and forget

3. *EVERY MARRIAGE HAS ITS OWN CHALLENGES*
Marriage is not bed of roses every shinning marriage has gone through its own test of fire

4. *EVERY MARRIAGE HAS DIFFERENT LEVELS OF SUCCESS*
We can never be equal, some will be far front and others far behind. To avoid marriage stresses, be patient, work hard and with time your marriage dreams shall come true

5. *TO MARRY IS TO DECLARE A WAR*
When you marry you enter in to a battle field. Be ready to fight to maintain your marriage zone.

6. *THERE IS NO PERFECT MARRIAGE*
There is no ready made marriage. Marriage is a hard work, volunteer yourself and perfect it daily

7. *GOD CANNOT GIVE YOU A COMPLETE PERSON YOU DESIRE*
He gives you, him or her inform of raw materials in order for you to mould what you desire

8. *TO MARRY IS TO TAKE A RISK*
You cannot predict what will happen after marriage, situation may change, so leave a room for adjustment

9. *MARRIAGE IS NOT A CONTRACT, IT IS PERMANENT*
Marriage needs total commitment, love is the glue that makes a couple stick together. Divorce starts in the mind

10. *EVERY MARRIAGE HAS A PRICE TO PAY*
There is no free love in marriage, You cannot love without giving a sacrifice

Daktari FEKI adaiwa kuua mgonjwa Singida Baada ya Kumfanyia Upasuaji wa Tezi Dume


Mkazi mmoja mkoani Singida anayedaiwa kuwa daktari feki anatuhumiwa kusababisha kifo cha mgonjwa, Israel Shabani (68) baada ya kumfanyia upasuaji wa tezi dume.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Alhamisi iliyopita saa mbili usiku nyumbani kwa mtuhumiwa baada ya kumfanyia Shabani upasuaji.


Alisema mtuhumiwa huyo anadaiwa alikuwa akifanya kazi katika vituo vya afya serikalini, lakini baada ya kuacha alijiita daktari na kuamua kutoa tiba ikiwamo ya upasuaji nyumbani kwake kinyume na sheria.


Baada ya kumfanyia upasuaji huo wa kienyeji, mgonjwa huyo alitokwa damu nyingi na kuwa katika hali mbaya.Mtuhumiwa alipobaini hali hiyo, alimtelekeza na kukimbilia kusikojulikana.

Alidai kuwa baada ya polisi kufanya upekuzi kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo, walikamata vifaa vingi vya tiba zikiwamo dawa za kutibu binadamu.

Maneno ya Demba Ba Baada ya Kutembelewa na Aliyemvunja Mguu



Lilikuwa ni tukio la kusikitisha pale mshambuliaji nyota wa zamani wa Newcastle na Chelsea Demba Ba alipovunjia mguu akiwa uwanjani kutekeleza majukumu yake.

Jina la Ba limekuwa kwenye vyombo vya habari baada ya kuvunjika mkuu wake wakati wa mchezo wa Shanghai derby.

Akicheza dhidi ya Shanghai SIPG, striker huyo wa Shanghai Shenhua alishuhudia mwish wake wa msimu pale mguu wake wa kulia ulipopinda mithili ya plastic laini.

Siku ya Jumanne, Sun Xiang alimtembelea Demba Ba hospitali ambapo pia Ba alizungumza na vyombo vya habari kwa mara ya kwanza tangu alipoumia.

Demba Ba: Nimefurahi timu imeshinda

Akizungumza na kituo cha television cha Chinese TV, Demba Ba alisema: “Ilikuwa ni siku ngumu (Jumapili) kwa upande wangu na timu nzima, lakini ninafurahi tulishinda.”

“Napenda kuwashukuru mashabiki wote ambao wanakuja kunijulia hali hospitalini.”

Imeripotiwa pia na vymbo vya habari vya China kwamba, Demba Ba amemsamehe Sun Xiang kwa kusema: “Msimlaumu, mimi naendelea vizuri.”

Hivi Ndivyo Mabilioni ya Pesa Yalivyotafunwa NSSF Mpaka Kusababisha Wakurugenzi Sita Kutumbuliwa UBADHIRIFU wa fedha na ukiukwaji wa taratibu na sheria katika usimamizi wa miradi kadhaa ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), vimeelezwa kuwa miongoni mwa sababu za kusimamishwa kazi wakurugenzi sita na mameneja watano wa shirika hilo. Vigogo hao walisimamishwa kazi juzi na Bodi ya Wadhamni ya NSSF inayoongozwa na mwenyekiti wake, Profesa Samwel Wangwe, kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za ubadhirifu, matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata kanuni, sheria na taratibu katika uwekezaji, usimamizi wa miradi, ununuzi wa ardhi na ajira katika shirika hilo. Waliosimamishwa ni Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi, Yacoub Kidula, Mkurugenzi wa Fedha, Ludovick Mrosso, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Chiku Matessa na Mkurugenzi wa Udhibiti, Hadhra na Majanga, Said Shemliwa. Wengine ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Hesabu za Ndani, Pauline Mtunda na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Cresentius Magori. Mameneja waliosimamishwa ni Meneja Utawala, Amina Abdallah, Meneja wa Uwekezaji, Abdallah Mseli na Meneja wa Miradi, John Msemo. Wengine ni Mhasibu Mkuu, John Davis Kalanje, Meneja Kiongozi Mkoa wa Temeke, Wakili Chedrick Komba na Meneja Miradi, John Ndazi. Inaelezwa kuwa baadhi ya ubadhirifu huo ulifanywa kupitia miradi ya usimamizi wa nyumba za kuuza zilizopo Mtoni Kijichi, Dar es Salaam, unaokadiriwa kufikia Sh bilioni 137.7. Katika ripoti ya mwaka ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu ukaguzi wa mashirika ya umma kwa mwaka wa fedha 2014/2015, imebainika kuwa ulikuwapo ukiukwaji mkubwa wa taratibu katika miradi hiyo. Taarifa hiyo ya CAG inaeleza katika ukurasa wa 165 na 166 kuwa Juni 30 mwaka 2015, Sh bilioni 79 za shirika hilo zilitumika katika ujenzi wa nyumba hizo ambazo ziliamuriwa kuuzwa ndani. Uamuzi huo ulitolewa badala ya kufuata maelekezo ya wasimamizi kwa kutumia benki au makampuni ya mikopo kama ilivyoelekezwa katika kanuni namba 13 ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na mwongozo wa uwekezaji wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Katika maoni yake kuhusu mradi huo, ofisi ya CAG iliishauri menejimenti ya NSSF kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo yanayotolewa na wasimamizi wake. “Kitendo chochote cha kutofuata maagizo kinatakiwa kuwasilishwa kwa maandishi kwa mdhibiti wa sekta na kukubaliana muda uliopangwa kwa ajili ya kufuatwa,” ilisema sehemu ya ripoti hiyo. Ukiukwaji mwingine wa sheria na taratibu unaotajwa kufanywa na vigogo hao, ni ununuzi wa ardhi bila ushindani kutoka kwa muuzaji mmoja, kwa gharama ya Sh bilioni 15.16. Taarifa hiyo ya CAG inaeleza kuwa NSSF ilipanga bajeti ya Sh bilioni 1.6 kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja kupitia zabuni za ushindani. “Hata hivyo, ilitumia chanzo kimoja katika ununuzi wa kiwanja kilichogharimu Sh bilioni 15.16. Nimegundua kwamba Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma haikujulishwa, kinyume cha kanuni namba 87 ya mwaka 2013 ya mamlaka hiyo inayohitaji kuwasilishwa taarifa za mkataba wa tuzo kwake, ndani ya siku saba kuhusu mchakato wa ununuzi endapo chanzo kimoja kilitumika,” inasomeka sehemu ya ripoti hiyo ya CAG. CAG aliishauri menejimenti ya NSSF kuzingatia mpango wake wa bajeti na kanuni za ununuzi wa umma za mwaka 2013, kuhakikisha ununuzi unafanyika katika ushindani ili kupata huduma kwa bei nafuu. Kutokana na hali hiyo, katika ripoti hiyo ya ukaguzi, CAG alieleza namna NSSF lilivyoingia ubia na Kampuni ya Azimio Housing Estate kuanzisha kampuni maalumu kwa jina la Hifadhi Bulders Limited. Katika mkataba huo, Azimio Housing Estate inatakiwa kuendeleza ekari 20,000 za ardhi zilizopo Kigamboni ambapo kwa hatua ya awamu itaaanza na ekari 300. “Katika ubia huu, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii linamiliki asilimia 45 ya hisa wakati Azimio Housing Estate inamiliki asilimia 55. Jumla ya gharama za mradi ni dola za Marekani milioni 653.3.44. “Ukaguzi wa hatimiliki umeonyesha kuwa Azimio Housing Estate inamiliki viwanja viwili, kiwanja chenye hatimiliki namba 81828 chenye ukubwa wa hekta 1.98 na chenye hatimiliki namba 105091 chenye ukubwa wa hekta 114.11 ambavyo vyote vinapatikana katika eneo la Rasi Dege,” ilieleza taarifa ya CAG. Pamoja na hali hiyo, CAG alisema kuwa hajaweza kupatiwa hatimiliki za ardhi ambayo Azimio iliahidi kutoa kama uchangiaji wa mtaji hali ambayo NSSF ililipa asilimia 20 ya fedha kama mtaji ambazo zilikuwa kwenye hatari ya kupotea. Licha ya kuibuliwa kwa hili, CAG alieleza kuwa Menejimenti ya NSSF ina udhaifu katika mifumo ya kifedha na kiuhasibu. Kwamba wana mfumo mkuu wa usimamizi wa rasilimali ambao unaweza kuunganishwa na mfumo wa usimamizi wa fedha ambao unakosa moduli ya uhasibu kwa ajili ya kuhifadhi taarifa za kifedha. DENI LA BIL 723.22 Katika taarifa hiyo ya CAG, inaelezwa kuwa NSSF iliikopesha Serikali katika miradi yake mbalimbali, lakini hata hivyo imekuwa hailipi madeni yake kwa muda mrefu. Kwamba hali hiyo imekuwa ikisababisha kuongezeka kwa limbikizo la riba na adhabu hadi kufikia asilimia 39 ya salio la Sh bilioni 729.22 kufikia Juni 2014. WAFANYAKAZI NA MADENI Shirika hilo lina utaratibu wa ndani wa kutoa mikopo kwa wafanyakazi wake, na ukaguzi umeonyesha kiasi cha Sh milioni 827.98 bado kinadaiwa kwa wafanyakazi ambao si waajiriwa tena wa NSSF. Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais John Magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau na kumteua kuwa balozi ingawa hadi sasa hajapangiwa nchi ya kwenda. Vilevile, mwanzoni mwa Machi mwaka huu, mrithi wa Dk. Dau, Dk. Carine Wangwe ambaye aliteuliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, uteuzi wake ulitenguliwa na Ofisi ya Rais Ikulu katika kile kilichoelezwa kuwa ulikiuka taratibu. KUHOJIWA TAKUKURU Wakati huohuo, taarifa zilizoifikia MTANZANIA jana, zilisema vigogo hao wameanza kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu suala hilo. Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola, alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, alisema yuko nje ya ofisi na akashauri atafutwe msemaji wa taasisi hiyo, Mussa Misalaba. Hata hivyo, Misalaba alipoulizwa, alisema hana taarifa na jambo hilo kwa sababu hakuwa ofisini. Bonyeza HAPA kudownload application ya UDAKU SPECIAL kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka 20 Jul



UBADHIRIFU wa fedha na ukiukwaji wa taratibu na sheria katika usimamizi wa miradi kadhaa ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), vimeelezwa kuwa miongoni mwa sababu za kusimamishwa kazi wakurugenzi sita na mameneja watano wa shirika hilo.

Vigogo hao walisimamishwa kazi juzi na Bodi ya Wadhamni ya NSSF inayoongozwa na mwenyekiti wake, Profesa Samwel Wangwe, kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za ubadhirifu, matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata kanuni, sheria na taratibu katika uwekezaji, usimamizi wa miradi, ununuzi wa ardhi na ajira katika shirika hilo.

Waliosimamishwa ni Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi, Yacoub Kidula, Mkurugenzi wa Fedha, Ludovick Mrosso, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Chiku Matessa na Mkurugenzi wa Udhibiti, Hadhra na Majanga, Said Shemliwa.

Wengine ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Hesabu za Ndani, Pauline Mtunda na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Cresentius Magori.

Mameneja waliosimamishwa ni Meneja Utawala, Amina Abdallah, Meneja wa Uwekezaji, Abdallah Mseli na Meneja wa Miradi, John Msemo.

Wengine ni Mhasibu Mkuu, John Davis Kalanje, Meneja Kiongozi Mkoa wa Temeke, Wakili Chedrick Komba na Meneja Miradi, John Ndazi.

Inaelezwa kuwa baadhi ya ubadhirifu huo ulifanywa kupitia miradi ya usimamizi wa nyumba za kuuza zilizopo Mtoni Kijichi, Dar es Salaam, unaokadiriwa kufikia Sh bilioni 137.7.

Katika ripoti ya mwaka ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu ukaguzi wa mashirika ya umma kwa mwaka wa fedha 2014/2015, imebainika kuwa ulikuwapo ukiukwaji mkubwa wa taratibu katika miradi hiyo.

Taarifa hiyo ya CAG inaeleza katika ukurasa wa 165 na 166 kuwa Juni 30 mwaka 2015, Sh bilioni 79 za shirika hilo zilitumika katika ujenzi wa nyumba hizo ambazo ziliamuriwa kuuzwa ndani.

Uamuzi huo ulitolewa badala ya kufuata maelekezo ya wasimamizi kwa kutumia benki au makampuni ya mikopo kama ilivyoelekezwa katika kanuni namba 13 ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na mwongozo wa uwekezaji wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Katika maoni yake kuhusu mradi huo, ofisi ya CAG iliishauri menejimenti ya NSSF kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo yanayotolewa na wasimamizi wake.

“Kitendo chochote cha kutofuata maagizo kinatakiwa kuwasilishwa kwa maandishi kwa mdhibiti wa sekta na kukubaliana muda uliopangwa kwa ajili ya kufuatwa,” ilisema sehemu ya ripoti hiyo.

Ukiukwaji mwingine wa sheria na taratibu unaotajwa kufanywa na vigogo hao, ni ununuzi wa ardhi bila ushindani kutoka kwa muuzaji mmoja, kwa gharama ya Sh bilioni 15.16.

Taarifa hiyo ya CAG inaeleza kuwa NSSF ilipanga bajeti ya Sh bilioni 1.6 kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja kupitia zabuni za ushindani.

“Hata hivyo, ilitumia chanzo kimoja katika ununuzi wa kiwanja kilichogharimu Sh bilioni 15.16. Nimegundua kwamba Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma haikujulishwa, kinyume cha kanuni namba 87 ya mwaka 2013 ya mamlaka hiyo inayohitaji kuwasilishwa taarifa za mkataba wa tuzo kwake, ndani ya siku saba kuhusu mchakato wa ununuzi endapo chanzo kimoja kilitumika,” inasomeka sehemu ya ripoti hiyo ya CAG.

CAG aliishauri menejimenti ya NSSF kuzingatia mpango wake wa bajeti na kanuni za ununuzi wa umma za mwaka 2013, kuhakikisha ununuzi unafanyika katika ushindani ili kupata huduma kwa bei nafuu.

Kutokana na hali hiyo, katika ripoti hiyo ya ukaguzi, CAG alieleza namna NSSF lilivyoingia ubia na Kampuni ya Azimio Housing Estate kuanzisha kampuni maalumu kwa jina la Hifadhi Bulders Limited.

Katika mkataba huo, Azimio Housing Estate inatakiwa kuendeleza ekari 20,000 za ardhi zilizopo Kigamboni ambapo kwa hatua ya awamu itaaanza na ekari 300.

“Katika ubia huu, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii linamiliki asilimia 45 ya hisa wakati Azimio Housing Estate inamiliki asilimia 55. Jumla ya gharama za mradi ni dola za Marekani milioni 653.3.44.

“Ukaguzi wa hatimiliki umeonyesha kuwa Azimio Housing Estate inamiliki viwanja viwili, kiwanja chenye hatimiliki namba 81828 chenye ukubwa wa hekta 1.98 na chenye hatimiliki namba 105091 chenye ukubwa wa hekta 114.11 ambavyo vyote vinapatikana katika eneo la Rasi Dege,” ilieleza taarifa ya CAG.

Pamoja na hali hiyo, CAG alisema kuwa hajaweza kupatiwa hatimiliki za ardhi ambayo Azimio iliahidi kutoa kama uchangiaji wa mtaji hali ambayo NSSF ililipa asilimia 20 ya fedha kama mtaji ambazo zilikuwa kwenye hatari ya kupotea.

Licha ya kuibuliwa kwa hili, CAG alieleza kuwa Menejimenti ya NSSF ina udhaifu katika mifumo ya kifedha na kiuhasibu. Kwamba wana mfumo mkuu wa usimamizi wa rasilimali ambao unaweza kuunganishwa na mfumo wa usimamizi wa fedha ambao unakosa moduli ya uhasibu kwa ajili ya kuhifadhi taarifa za kifedha.



DENI LA BIL 723.22

Katika taarifa hiyo ya CAG, inaelezwa kuwa NSSF iliikopesha Serikali katika miradi yake mbalimbali, lakini hata hivyo imekuwa hailipi madeni yake kwa muda mrefu.

Kwamba hali hiyo imekuwa ikisababisha kuongezeka kwa limbikizo la riba na adhabu hadi kufikia asilimia 39 ya salio la Sh bilioni 729.22 kufikia Juni 2014.


WAFANYAKAZI NA MADENI

Shirika hilo lina utaratibu wa ndani wa kutoa mikopo kwa wafanyakazi wake, na ukaguzi umeonyesha kiasi cha Sh milioni 827.98 bado kinadaiwa kwa wafanyakazi ambao si waajiriwa tena wa NSSF.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais John Magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau na kumteua kuwa balozi ingawa hadi sasa hajapangiwa nchi ya kwenda.

Vilevile, mwanzoni mwa Machi mwaka huu, mrithi wa Dk. Dau, Dk. Carine Wangwe ambaye aliteuliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, uteuzi wake ulitenguliwa na Ofisi ya Rais Ikulu katika kile kilichoelezwa kuwa ulikiuka taratibu.


KUHOJIWA TAKUKURU

Wakati huohuo, taarifa zilizoifikia MTANZANIA jana, zilisema vigogo hao wameanza kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu suala hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola, alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, alisema yuko nje ya ofisi na akashauri atafutwe msemaji wa taasisi hiyo, Mussa Misalaba.

Hata hivyo, Misalaba alipoulizwa, alisema hana taarifa na jambo hilo kwa sababu hakuwa ofisini.

Tuesday, July 19, 2016

Ndugu wa mtanzania aliyewekwa rehani kwa unga Pakistan wazungumza

Baada ya wiki hii katika mitandao ya kijamii kusambaa video inayomuonyesha kijana mtanzania anayedaiwa kuwekwa rehani nchini Pakistan kutokana biashara ya unga, ndugu wa kijana huyo anayetambulika kwa jina la ‘Adamu Akida’ wamezungumza.

IMG_20160719_112117

Akiongea na gazeti la Mtanzania kaka wa Adamu aliyejitambulisha kwa jina la Hemed Abdallah (si jina lake halisi) alisema miezi minane iliyopita, Adamu alikwenda kwa kaka yake ambaye ni mtoto wa mama yake mdogo aliyetambulika kwa jina la Juma, na kuomba msaada wa mtaji kwani kazi yake ya kinyozi haikuwa ikilipa na hali ya maisha ilikuwa ngumu.
Alisema baada ya kueleza shida yake hiyo, kaka yake huyo (Juma) alimuhoji kama yupo tayari kwa ajili ya kutafuta maisha nje ya nchi, na Adamu alikubali kufanya kazi ya aina yoyote ili mradi aweze kupata pesa.
“Adamu kwa sasa ameshikiliwa kwa muda wa miezi minane, hatujui kama alikuwa ameingia katika janga hili hadi pale tulipoona video zake katika mitandao ya kijamii. Hapa aliyepo ni baba yake mdogo, Kessy Baharia na baba yake mzazi yupo Bagamoyo Mlingotini, ndiko anakoendelea na maisha yake.
“Awali alikwenda kwa kaka yake mtoto wa mama yake mdogo anaitwa Juma na kuomba asaidiwe mtaji kwani amekuwa na maisha magumu sana. Baada ya hali hiyo aliambiwa kuna safari ya kwenda Pakistan ambayo waliondoka wakiwa wameambatana watu watatu pamoja na Juma na kijana mwengine ambaye jina lake limenitoka, ila anaishi Kinondoni.
“Walipofika kule, Juma akachukua mzigo akiwa na yule kijana wa Kinondoni, huku Adamu akiachwa Pakistan kwa maelezo kuwa baada ya siku tano atakuja nchini na mzigo mwingine. Muda wote hata tukihoji alipo Adamu tunaambiwa yupo anaendelea na kazi huko aliko ana angerudi mwezi wa tisa nane.
“Sasa hii video ndiyo imetupa picha halisi ya Adamu, maskini sijui kama tutampata akiwa hai. Hata hivyo kwa kipindi cha hivi karibuni, tulikuwa tukishangazwa na mwenendo wa Juma kwani amekuwa na fedha nyingi sana hadi kufikia kuwajengea nyumba dada zake pamoja na kuwanunulia magari,” alisema Abdallah huku akibubujikwa na machozi.
Mke wake
Inaelezwa kuwa mke wa Adamu ambaye alikuwa akiishi Mtaa wa Sunna, Magomeni, alihamia Kijitonyama.
Kwamba alihamishwa na shemeji yake, Juma ambaye ndiye aliyempangia nyumba nyingine Kijitonyama.
“Katika suala hilo, tuna shaka kuwa hata mke wa Adamu anajua kinachoendelea, maana miezi mitatu iliyopita alihama Magomeni na kuhamia Kijitonyama, tena huku akisema mume wake karibu anarejea nchini.
“Lakini baada ya video kuanza kuonekana, sasa hata kupatikana hapatikani, na hatujui amehamia nyumba gani huko Kijitonyama,” alisema Abdallah.
Serikali ya Mtaa
Akizungumza na Mtanzania, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Idrissa, Issa Mpangile, alisema kuwa jana askari kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi walifika katika ofisi yake na kumtaka waongozane kwenda katika nyumba ya baba mdogo wa Adamu.
Alisema walipofika nyumbani kwa Kessy Baharia, ambaye ndiye baba mdogo wa Adamu, polisi walichukua maelezo yake na baadaye wakarudi katika ofisi ya Serikali ya Mtaa kuchukua maelezo ya mwenyekiti huyo.
Akizungumza kuhusu kijana huyo, Mpangile alisema kuwa ni mzaliwa wa mtaa huo, lakini baadaye alihamia Mtaa wa Suna ambao ni jirani na Mtaa wa Idrissa, Kata ya Magomeni.
Alisema wakati kijana huyo anahama mtaa huo, alikuwa bado ni kinyozi na hakuwa na rekodi ya kusafiri kwenda nje ya nchi.
“Wakati Adamu anahama Mtaa wa Idrissa, alikuwa bado ni kinyozi na hakuna rekodi kwamba alikuwa anasafiri nje ya nchi,” alisema Mpangile.
Mpangile alisema kwa mujibu wa Baharia, baba wa kijana huyo anayejulikana kwa jina la Akida, amesikia habari za mtoto wake na kwamba atakwenda kuripoti kituo cha polisi.
Naye mama mdogo wa Adamu, aliyetambulika kwa jina la Khadija Katundu, alikiri maofisa wa polisi kumuhoji mume wake.
Alisema wameendelea kutoa ushirikiano kwa watu wanaofika nyumbani kuhoji kuhusu suala hilo, na kwamba wanaamini ufumbuzi utapatikana.
Serikali yahaha
Baada ya taarifa hizo kuripotiwa na gazeti hili jana, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi wanafanya mawasiliano na Serikali ya Pakistan ili kuangalia namna ya kumwokoa Adamu katika mikono ya maharamia hao.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Msemaji wa Polisi, Advera Bulimba, alisema tayari wamepata taarifa dhidi ya Mtanzania huyo.
“Kwa sasa tunafanya mawasiliano na wenzetu wa Pakistan tuone namna ya kumtoa kijana huyo katika mikono ya hao watekaji, na tukikamilisha hilo tutatoa taarifa rasmi juu ya jambo hili,” alisema Advera.
Wakati hayo yakiendelea, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, kupitia mmoja wa maofisa wa idara ya habari ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini, alisema wamepata taarifa ya tukio hilo, na sasa wanafanya mawasiliano na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Source: Mtanzania

Majina ya wachezaji 10 watakaowania tuzo ya mchezaji bora Ulaya mwaka 2015/2016

Shirikisho la soka barani Ulaya limetangaza majina ya wachezaji 10 watakaowania tuzo ya mchezaji bora Ulaya kwa msimu wa mwaka 2015/2016, majina hayo 10 yametangazwa huku Cristiano Ronaldo akipewa nafasi ya kushinda tuzo hiyo itakayotolewa Agosti 25 mwaka huu.

mchezaji-bora-Ulaya

Hi ndiyo orodha ya majina 10 ya wachezaji wanao wania tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya msimu wa 2015/16
Cristiano Ronaldo (Real Madrid & Ureno)
Gareth Bale (Real Madrid & Wales)
Gianluigi Buffon (Juventus & Italia)
Antoine Griezmann (Atlético Madrid & Ufaransa)
Toni Kroos (Real Madrid & Ujerumani)
Lionel Messi (Barcelona & Argentina)
Thomas Müller (Bayern München & Ujerumani)
Manuel Neuer (Bayern München & Ujerumani)
Pepe (Real Madrid & Ureno)
Luis Suárez (Barcelona & Uruguay)

Mtoto wangu wa kike ataitwa Karma – Wema

Malkia wa filamu Wema Sepetu bado hajakata tamaa kuhusu kupata mtoto licha ya kukatishwa tamaa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii kutokana na uzazi wake kuwa mgumu.

wema

Muigizaji huyo ambaye alianzisha mfumo wa APP na SMS ambao unatoa taarifa zake mbalimbali kwa mashabiki juu ya maisha yake, tayari umeanza kutoa taarifa mbalimbali kuhusu maisha yake.
Kupitia mfumo huo, Wema amesema angependa mwanae wakiume ampatie jina la Karma.
“Mtoto wangu wa kiume ataitwa Karma,” alisema Wema. “Bado sijafikiria jina nitakalo mpa mtoto wangu wa kiume japo namtaka sana mtoto wa kwanza awe wa kiume, Mungu anajua,” alisema Wema.
Pia kupitia system hiyo, Wema amewashukuru mastaa wenzake wa filamu ambao walimsupport katika show yake ya ‘The Black Tie’.


FAIZA Ally Amfungukia Mchumba Mpya wa Mh Sugu..Adai Anahonga Mashemeji na Mama Mkwe



Faiza Ally Kamfungukia Mrembo anayesemekana ndio mchumba wa Mh Mr Sugu Kwa Sasa Anaitwa Happy...
Soma Hapa:
Simpati Kwa lipi huyo happy - makengeza? Au Kwa sababu Ana Fany kazi biuro Au Kwa sababu Na baba Sasha wamefanana sura ? Simpati Kwa sababu kila wiki anatuma Mbeya Samaki? Simpati Kwa sababu Ana mfupi mweusi mbaya Au simpati Kwa sababu Ana tumia nguvu Na hela KWENYE mapenzi ? Au simpati Kwa sababu mweusi Ana vidole Kama tangawizi? Mkisema simpati mna maanisha nn hasa ? Au simpati Kwa sababu hazai ? Simpati kivipi labda tuwekane Sawa ! Siwaelewi ....? Nielewesheni? Au simpati Kwa sababu Ana honga mashemeji Na mama mkwe yaani kivipi sielewi? Haha nyie mnao SEMA simpati naombeni majibu simpati kivipi ? Au simpati Kwa sababu amenuna gari kasema kanunuliwa ? Siwaelewi simpati kivipi ? 

PAUL Makonda Adai Mashoga Dar es Salaam Wanafanya Mpango wa Kumwangamiza



MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema tangu alipotangaza kuanza kukamatwa kwa mashoga, amebaini kuna mkakati unawaohusisha watu hao zaidi ya 150 kutaka kumwangamiza.

Kauli hiyo aliitoa jana Dar es Salaam baada ya kumaliza mahojiano katika kituo cha redio Clouds FM, ambako alikuwa akifafanua hoja na changamoto mbalimbali za mkoa wake.

Alisema kuwa baada ya kubainika kwa mipango hiyo, mashoga wanane wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi.

“Lazima watu wajue jitihada na harakati za kusimamia katiba na usawa hapa nchini. Hakuna anayezipenda, vita inakuwa kubwa… Nimebaini kuwa mashoga zaidi ya 150 waliketi katika baa moja Kinondoni wakipanga njama za kunimaliza kwa namna moja ama nyingine, lakini kutokana  na taarifa za kiintelijensia, watu kadhaa, wengi wao wakiwa ni mashoga wameshakamatwa,” alisema Makonda.

Katika hatua nyingine, Makonda aliwatolea uvivu watu wanaosambaza ujumbe wa tofauti juu ya maagizo yake katika mitandao ya kijamii, ikiwamo kutengeneza akaunti feki.

“Kwanza wanapaswa kujua kuwa sina akaunti ambayo inaanza na cheo changu, hivyo akaunti zote zangu zimeandikwa kwa jina langu Paul Makonda si vinginevyo, hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo,” alisema Makonda.

Aliweka wazi kuwa kuna agizo batili lililowekwa katika mitandao ya kijamii, akidaiwa kusema kuwa watu wasiokuwa na kazi watakwenda jela, lakini ukweli ni kwamba ameagiza wenyeviti wa Serikali za mtaa kuhakikisha kuwa wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa nyumba kwa ajili ya usalama wa maeneo wanayoishi.

Aidha Makonda alisisitiza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo, kamwe Hatoacha kupambana na mafisadi katika halmashauri zote tatu za mkoa wake, pamoja na wauza unga, wafanyabiashara wa shisha na mashoga.

Monday, July 18, 2016

Calvin Harris na Tinashe ni wapenzi!

Calvin Harris amepata mrembo mwingine, baada ya kuachana na Taylor Swift.
calvin-harris-tinashe

Chanzo kimeimbia Page Six kuwa Dj huyo tajiri kwa sasa ana uhusiano wa kimapenzi na Tinashe.
Kimedai kuwa wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja siku za hivi karibuni.
Tinashe na Harris walikutana studio mwaka 2014 walipofanya wimbo ‘Dollar Signs.’ Waliwahi pia kudaiwa kuandika nyimbo za Rihanna.
“They stayed in touch and recently started hanging out again,” chanzo kilisema. Jumamosi iliyopita wawili hao walionekana huko Nobu Malibu.
“It was clearly a date. They were super close,” kiliongeza chanzo hicho.

Jux: African Boy inanilipa kuliko nilivyotarajia

Jux amedai kuwa brand ya African Boy imegeuka kuwa kitu kinachomuingizia fedha nyingi kwa sasa

.13108563_570785076419832_1652219953_n
Amedai kuwa jinsi nguo zake zinavyofanya vizuri kwa sasa kumemfanya awe na mipango mikubwa zaidi siku za usoni.
“Kwa muda mfupi African Boy imenipa pesa ambayo naweza kusema kwamba imenisaidia vitu vingi sana. Ni kitu ambacho kinafanya vizuri sana, nikileta mzigo sasa hivi in two weeks au one week hata ukiwa mkubwa vipi, mara nyingi sana nakuwa nimemaliza,” Jux ameiambia Bongo5.
13256692_131402337267978_416813564_n

Anasema mpango wake ni kuwa na duka kubwa litakalokuwa likiuza bidhaa zake tu. Kwa upande wa viatu vya brand yake, amedai kuwa aliletewa sample lakini hakuridhishwa na kiwango chake kwakuwa vitakuwa vikiuzwa kwa bei kubwa kidogo.
Amesema kiatu chake kitauzwa kwa shilingi laki mbili na kwamba kitakuwa na ubora wa hali ya juu.

Muziki umenipa heshima kubwa – Ben Pol

Mkali wa muziki wa R&B Bongo, Ben Pol amedai kuwa muziki umempa heshima kubwa kwenye maisha yake kwa kuweza kuisaidia familia yake.
Ben Pol

Wimbo wa ‘Moyo Mashine’ wa Ben Pol umezidi kufanya vizuri kwenye Radio na TV kubwa Afrika.
Muimbaji huyo ameiambia BBC Radio kuwa kwa sasa muziki umemsaidia kusomesha wadogo zake wawili kwenye shule nzuri.
“Wadogo zangu wapo wawili nimewatoa shule ambazo naona siyo nzuri nimewapeleka shule nzuri wanasoma nina wahudumia kila kitu. Wazazi wangu sasa hivi wameshakuwa watu wazima kidogo ufanisi umepungua mimi ndio nipo responsible,” amesema Ben Pol.
Aidha staa huyo ametoa sababu ya kuupa wimbo wake mpya jina la ‘Moyo Mashine’ ni kutokana na moyo umekuwa ukifanya kazi kubwa kwenye mwili kama mashine

Sare ya TP Mazembe v Mo Bejaia yazidi kuishindilia Yanga mkiani



TP Mazembe imejiongezea pointi moja baada ya kupata sare ya bila kufungana dhidi ya wenyeji wake Mo Bejaia katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

TP Mazembe walikuwa wageni wa Bejaia katika mechi ngumu usiku wa kuamkia leo na watakuwa na furaha baada ya kupata pointi hiyo moja muhimu.

Sare hiyo imeihakikishia TP Mazembe kufuzu hatua ya nusu fainali kwa asilimia 90 kwa kuwa kama itashinda mechi moja katika mechi tatu zilizobaki basi itakuwa ina uhakika wa asilimia 100.

Lakini sare hiyo, imezidi kudidimiza matumaini ya Yanga kuamka angalau na kupata pointi zitakazoiwezesha kubadili mambo kwa kuwa ina pointi moja tu baada ya kucheza mechi tatu ikipoteza mbili na kupata sare moja tu dhidi ya Medeama.


TP Mazembe inaendelea kuongoza kundi hilo ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Bejaia yenye tano, Medeama ina mbili na Yanga inaburuza mkia na pointi hiyo moja.

Breaking News Wakurugenzi wote wa NSSF wamesimamishwa kazi, kupisha uchunguzi wa idara zao katika shirika hilo.



BODI ya wakurugenzi ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limewasimamisha kazi wakurugenzi sita na meneja watano na Mhandisi mmoja kufuatia matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata sheria na kanuni.

Kwa mujibu wa taafia iliyotolewa leo na Mkurugnezi Mkuu wa NSSF,  Profesa Godius Kahyarara imesema hatua ya kuwasimamisha kazi wakurugenzi na mamenja hao inafuatia kikao cha bodi chini ya uenyekiti wa  Prefesa Samweli Wangwe kilichokaa kuanzia Ijumaa iliyopita.

“Bodi imeagiza  kusimamishwa kazi Wakurugenzi , Mameneja watano na Mhandishi mmoja ili kupisha uchunguzi ili kubaini wahusika katika tuhuma za ubadhirifu, matumizi mabaya ya ofisi na kutofuata kanuni, sheria na utatibu katika uwekezaji,  usimamizi wa miradi na manunuzi ya ardhi na ajira,” alisema Profesa Kahyarara.

Aliwataja wakurugenzi hao ni Mkurugenzi wa mipango, Uwekezaji na Miradi, Yakub Kidura, Mkurugenzi wa fedha, Ludovick Mrosso, Mkurugenzi wa rasilimali watu na utawala, Chiku Matessa, Mkurugenzi wa Udhibiti,Hadhara na Majanga, Sadi Shemliwa, Mkurugenzi Mahesabu ya ndani, Pauline Mtunda na Mkurugenzi wa Uendeshaji,  Crescentius Magori.

Aidha Aliwataja mameneja waliosimamishwa ni pamoja na Meneja wa utawala, Amina Abdallah, Meneja wa Uwekezaji, Abdallah Mseli, Meneja Miradi, Mhadisi,John Msemo, Mhasibu Mkuu, Davis Kalanje, Meneja kiongozi mkoa wa Temeke, Wakili,  Chedrick Komba na Mhadisi John Ndazi.

Awali amedaiwa kuwa baadhi ya wakurugenzi na mameneja waliosimamishwa, leo wamefikishwa katika kituo cha polisi cha kati Dar es Salaam kwa mahojiano kufuatia tuhuma hizi zinazowakabili.

a wakurugenzi wote wa NSSF wamepigwa chini leo na wanne kati yao wako chini ya ulinzi.

DJ JOH wa 93.1 Marekani acheza Ngoma za Diamond!



Haya sasa naona taratibu ule ubishi wa kuwa nyimbo za Afrika hasa Tanzania hazichezwi kwenye vituo vya Radio za Marekani unaelekea kuisha!

Dj Joh wa 93.1 Marekani akihojiwa na Millard Ayo amezungumzia nafasi ya wasanii wa Afrika kusika katika vituo vya Radio vya marekani!! Amelezea Mengi lakini amekiri mara ya kwanza ili apate hiyo kazi ilibidi adanganye na alikataa kuwa yeye si mtanzania kutokana na ubaguzi lakini baadae alikuja kukubari kuwa ni mtanzania baada ya kazi zake kuanzwa kupendwa! Alienda Marekani kwa ajiri ya kusoma lakini alifika hatua akaanza kuwa Dj lakini hakuruhusiwa kuplay nyimbo za kiafrika kwani hakuwa anaruhusiwa!!

Anasema yeye ni anapenda Afro Pop na anaupenda sana mziki wa Diamond!!!! Kwa mara ya kwanza alijitosa na kuanza kuplay nyimbo za akina P-squre,Wizkid na Diamond!!! Anasema siku hiyo alipokea comments nyingi sanaaa zilizo mpongeza na kufanya yeye kuongeza juhudi ya kuplay nyimbo za kiafrika hasa Za diamond

Anasema siku ambayo hatoisahau ni siku Alio play nyimbo za Diamond na baada ya kipindi alipigiwa simu na Mtu ambae ni Mmarekani na alimuuliza kuwa Diamond kamfahamia wapi ndipo Dj Joh alipo sema yeye ni mtanzania na anamfahamu Diamond!!! Yule mmarekani alimwambia yeye Kwa Afrika Diamond ndo Msanii anaye mvutia na kwenye Gari yake muda mwingi huwa anasikiliza nyimbo za Diamond japo haelewi lugha!!! Dj Joh amesema kuwa Yule mmarekani alimwambia wiki ijayo nina harusi yangu na ninaomba uje Uwe Dj kwenye Harusi yangu na Nyimbo za Diamond uwe nazo nyingi!! Hapo Dj Joh anasema alifurahi nakuona kuwa mziki wetu sasa unakuwa!! Dj Joh amesema number don't lie kwani ni wengi walio mpigia simu na kumpongeza na kumtaka kumjua Diamond!!!

Mbali na hilo kuna siku Diamond alipost video ilionesha sehemu fulani Marekani watu wapo kwenye shuhuri wakisikiliza Nasema nawe!! Millard ayo ameongeza na kusema kuwa pia kuna kituo kingine cha Radio marekani kinachoitwa CSB nacho hucheza nyimbo Za Diamond!!!

Ni wazi sasa mziki wetu umefika mbali!!! Kuna siku niliwahi sema Diamond nyimbo yake na Neyo itachezwa sana kwenye Vituo vya Radio vya Marekani lakini watu walinipinga sana humu na sasa limeanza kujidhihirisha Kabla hata ya hiyo collabo

JOKATE Aweka Silaha Chini na Kunyoosha Mikono Kwa Ex Wake Diamond Platnumz



Diamond Platnumz anazidi kuwa karibu tena na maex wake. Jacqueline Wolper, Wema Sepetu hawana noma naye tena – na sasa Jokate Mwegelo!

Ya Jokate ina nguvu zaidi kwakuwa kwa sasa ana uhusiano na hasimu wake kiburudani, Alikiba na hiyo ni ishara kuwa uadui kati ya Diamond na Kiba umebaki kwa mashabiki tu.

Mrembo huyo amempongeza Diamond kwa uwezo wake mkubwa wa uchezaji wa style mpya kwenye hit single yake, Kidogo.

Akipost kipande cha video Instagram kikimuonesha Diamond na dancers wake wakifanya mazoezi kwa wimbo huo, Jokate ameandika:
You just took choreography ya East African tracks to another sphere, inspirational is an understatement. Moves za kwenye huu wimbo. I can’t even hata.”
Jojo pia anatamani amuone Chibu na Kiba kwenye ngoma moja.
“Naendelea kusubiri siku utakayo fanya kazi na team kiba tho- kiroho safi 😊. Hongera kwa kazi nzuri dogo @diamondplatnumz.”

Mapokezi ya post hiyo yana mchanganyiko wa hisia. Ila wengi wamempongeza.

Mara ya mwisho Jokate anamuongelea Diamond ilikuwa ni malalamiko aliyommwagia kwa kumuita mswahili na mdhalilishaji wa wanawake.
Powered By Blogger