Friday, July 22, 2016

MICHEZO Dalili nyingine ya kuwa Paul Pogba atatua Man United msimu huu



Klabu ya Manchester United inayofundishwa na kocha mreno kwa sasa Jose Mourinhoimerudi kwenye headlines baada ya July 21 kutoa namba za jezi watakazovaa wachezaji wake kwa msimu wa 2016/2017, Man United wametangaza namba hizo za jezi na kuiacha namba ambayo inaaminika kuwa katengewa Paul Pogba.
Man United ambayo usiku wa July 20 iliripotiwa na na The Sun kuwa imekubaliana naJuventus ya Italia kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba kwa dau la pound milioni 105, inatajwa kuacha jezi namba 6 wazi, kitu ambacho kinatsirika kuwa ni namba ya jezi ambayo kawekewa Paul Pogba.
Manchester-United-Squad-Numbers-1024x1024
Wachezaji wapya wa Man United wote washapewa namba za jezi kama Zlatan Ibrahimovic atavaa jezi namba 9 iliyokuwa inavaliwa na Anthony MartialEric Baillyatavaa jezi namba 3 na Henrikh Mkhitaryan atavaa jezi namba 22. Pogba wakati anaondoka Man United 2012 alikuwa akivaa jezi namba 42.





Man United yaweka hadharani namba za jezi za wachezaji wao, namba 6 ni ya Pogba

Timu ya Manchester United imeweka hadharani namba ya jezi za wachezaji wao watakazozitumia kwa msimu wa mwaka 2016/2017.
wit-the-kids

Mshambuliaji mpya aliyesajiliwa hivi karibuni kwa uhamisho huru, Zlatan Ibrahimovic amekabidhiwa jezi yenye namba aliyozoea kuvaa muda mrefu yenye namba 9 iliyokuwa ikivaliwa na Antonio Martial klabuni hapo na sasa mchezaji huyo atakuwa anavaa jezi yenye namba 11 iliyokuwa ikivaliwa na nguli wa timu hiyo Giggs na kinda Januzaj.
Aidha kwenye orodha iliyotolewa na timu hiyo inaonyesha kuwa jezi namba 6 haijapata mvaaji huku kukiwa na taarifa kuwa imewekwa maalumu kwa kiungo Paul Pogba anayetarajiwa kutua klabuni hapo kwa uhamisho utakaoweka rekodi ya dunia wa paundi milioni 100.


Julen Lopetegui atangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Spain


Kocha wa zamani wa FC Porto, Julen Lopetegui ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya Spain akirithi mikoba ya Kocha Vicente Del Bosque aliyeondoka baada ya kufanya vibaya katika michuano ya Euro 2016 France.

2CDC2EB400000578-0-image-a-20_1443449279840

Julen,49, ambaye aliwahi kuwa mchezaji alikuwa kipa, amewahi pia kufundisha timu ya Taifa ya Spain chini ya miaka 19 na Chini ya miaka 21.


Bill Nas akana kufanya biashara haramu

Msanii wa Hip Hop Bongo, Bill Nas amekuwa akihusishwa na biashara haramu kutokana na kushoot video kali na za gharama tofauti na hela aliyoipata mpaka sasa kwenye muziki wake.
Billnass

Rapper huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, “Wasanii wengi hatupendi kuwekeza kwenye vitu vyetu.”
“Mimi nasoma biashara na elimu ya kwanza unapopata hela kwanza wekeza, unasave halafu kile kinachobakia unaweza uka-spend. Kwahiyo mimi bado nawekeza kwenye muziki wangu bado sijaanza kuspend kwa sababu naipenda kazi yangu,” ameongeza.
“Hata kwenda kushoot video Afrika Kusini nina risk sana kwa sababu siyo kama hela hizo zinarudi.”
Mpaka sasa Bill Nas ameshaachia nyimbo tatu huku wimbo wake wa ‘Chafu Pozi’ ukizidi kufanya vizuri kwenye radio na TV.


Zuio la Mikutano ya Kisiasa ni Kumyima Mwanchi Uhuru wa Haki ya Kujumuika- Kijo Bisimba.



Serikali imetakiwa kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ambazo zimeonekana kuwa kandamizi ikiwepo ile sheria za vyombo vya habari ambazo zinakandamiza uhuru wa vyombo vya habari pamoja na waandishi wenyewe.

Akitoa ripoti ya nusu mwaka mbele ya wanahabari kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa vyombo vya habari havifanyi kazi kwa uhuru kwani zipo sheria ambazo bado ni kandamizi.

”Vyombo vya habari bado havina uhuru kwani sheria kandamizi bado zinatumika mfano, gazeti la mawio kufungiwa na kutakiwa kutoandika nakala zake hata kwenye mitandao bila sababu maalumu”.Ilielezwa katika ripoti ya kituo hicho

Aidha ripoti hiyo ya miezi sita imesema kuwa wananchi bado wananyimwa haki zao za msingi  ikiwa ni pamoja na  kunyimwa haki ya habari kwasababu  serikali imeamua kutorusha matangazo ya bunge kwa sababu mbalimbali ambazo zinakinzana.

Katika ripoti hiyo pia imegusa haki za kujumuika ambapo kituo hicho kimesema matamko ya jeshi la polisi hasa katika kuzuia mikutano ya vyama imeonekana  kupendelea chama tawala huku vyama vya upinzani  vikiwa vinakandamizwa.

”Mfano mkutano wa Chadema shinyanga ulipewa vibali vyote lakini baadae ukaja kutawanyishwa kwa kutumia nguvu mpaka mabomu, aidha ACT walikuwa na kongamano la kuchambua bajeti lakini jeshi la polisi walizuia lakini wakati huo huo CCM walikubaliwa kufanya mkusanyiko” Ilieleza semu ya ripoti ya Kijo Bisimba.

Pamoja na hayo ripoti hiyo imetoa mapendekezo kwa Serikali  ikiwa kuboresha sheria hizo kandamizi kwa wananchi pamoja na kuachia vyombo vya habari kufanya kazi zake pasipo kuingiliwa sambamba na Vyama vya siasa kupewa haki sawa.

Maalim Seif kutinga Mahakama ya ICC leo Kuwashitaki Viongozi wa Serikali



Chama cha Wananchi (CUF) kimesema katibu wake mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad leo atakwenda katika Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) kuwashtaki viongozi wa Serikali kwa madai walitumia mamlaka yao vibaya wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kisha kuwatesa, kuwakamata na kuwapiga wafuasi wa chama hicho bila makosa.

Chama hicho kikuu cha upinzani Zanzibar, kimesema taratibu zote za kufungua mashtaka hayo zimeshakamilika, ikiwa ni pamoja na kuweka wakili.

Mei 22 mwaka huu, chama hicho kilizindua ripoti yake ya uvunjwaji wa haki za binadamu Zanzibar wakati wa uchaguzi huo na kutangaza azma yake ya kwenda ICC kuwashtaki Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema mpango huo umekamilika na Maalim Seif ambaye yuko nje ya nchi kwa ziara ya kueleza alichodai ‘figisufigisu’ zilizotokea katika uchaguzi mkuu, ataweka wazi kila kitu kilichotokea na jinsi ukiukwaji wa demokrasia ulivyoshika kasi nchini.

Mazrui alimtuhumu IGP Mangu kuwa anatumiwa na CCM kuwakamata viongozi wa CUF ili wasitimize azma yao ya kueleza ukweli wa yaliyotokea katika uchaguzi, huku akimtaka afute azma yake ya kumkamata Maalim Seif kwa maelezo kuwa “ataitumbukiza Zanzibar kwenye machafuko”.

Siku tano zilizopita, IGP Mangu wakati akihojiwa na Azam TV alisema Jeshi la Polisi wakati wowote litamburuza mahakamani Maalim Seif kwa kuhamasisha uchochezi Zanzibar. Iwapo CUF itatekeleza azima hiyo, itakuwa tukio la kwanza kwa Tanzania kupeleka viongozi wake kwenye mahakama hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na naibu wake, William Ruto wameshafikishwa huko, lakini kesi dhidi yao zilikosa nguvu na kuondolewa.

Katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Salim Jecha Salim alifuta matokeo ya rais, wawakilishi na madiwani Oktoba 28, mwaka jana siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa mbio za urais.

CUF ilidai kuwa ilishinda uchaguzi huo na Jecha alipotangaza uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu, chama hicho kilijitoa na hivyo CCM kushinda viti vyote.

Mazrui ambaye aliambatana na viongozi wengine wa chama hicho alisema: “Mpango wa kuishawishi dunia kuwachukulia hatua wahusika wote wa ukiukwaji wa haki za binadamu na uvunjwaji wa demokrasia uko palepale, hautasitishwa kwa vitisho vyovyote.

 “Lengo ni kuhakikisha unyama dhidi ya raia wasio na hatia unakomeshwa na uzingatiwaji wa sheria za nchi unatamalaki. Tunawaambia polisi kuwa tumechoshwa na figisufigisu maana zitazaa timbwiri.”

Mazrui alisema wanaotaka kuzuia mpango wa CUF kueleza ukweli na kwenda ICC, wanaandaa utaratibu wa kumkamata Maalim Seif aliyedai; “Ni kipenzi cha Wazanzibari”, akisisitiza kuwa jambo hilo ni hatari kwa sababu litaivuruga Zanzibar.

Akifafanua zaidi kile alichokiita mikakati ya CCM kupitia kwa IGP Mangu kuficha ukweli, Mazrui alidai kuwa polisi wamekuwa wakiwakamata wanachama wa CUF mara kwa mara.

"Niongeavyo hapa wanachama zaidi ya 400 wa CUF wamekamatwa na wengine wapo nje wa dhamana,” alisema.

Alisema ni jambo la ajabu kuona IGP Mangu akishindwa kutoa kauli yoyote baada ya Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DDCI), Salum Msangi kuwatishia mawakili kuwatetea wananchi wanaokamatwa kwa tuhuma  mbalimbali.

Alisema viongozi wa CUF hawatatishwa wala kunyamazishwa katika kudai haki ya ushindi wa Wazanzibari kutokana na uamuzi wao wa uchaguzi mkuu.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Shaweji Mketto alisema endapo IGP Mangu ataendelea kuwatisha viongozi wa CUF, watajipanga kwenda kumtembelea ofisini kwake.

IGP Mangu ajibu
Alipoulizwa kuhusu kauli za CUF, IGP Mangu alisema tayari ameshatoa msimamo wa Jeshi la Polisi na walichokifanya viongozi wa chama hicho ni kumjibu tu.

“Ukipendwa sana ukafanya uhalifu tukuache? Tukikutuhumu unafanya makosa tutakukamata hatuwezi kuogopa umaarufu wako,” alisema huku akisisitiza kuwa jalada kuhusu Maalim Seif lipo kwa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka).

“Umesema hao CUF wamesema kuna wanachama wao wamekamatwa, sasa wamekueleza hao wanachama ni kina nani?… kama wamekamatiwa Zanzibar wapo maofisa wa polisi wa mikoa wanaoweza kuzungumzia hilo huko Zanzibar.”

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema: “CCM hatuwezi kujiingiza katika hoja za IGP na CUF tumewaachia wenyewe. Kwa sasa tupo katika maandalizi ya kuhakikisha Rais (John) Magufuli anashinda kwa kishindo kuwa mwenyekiti wa CCM.” Alisema chama hicho hakina sababu ya kutumia Jeshi la Polisi kukandamiza wanachama na viongozi wa CUF.

Nay wa Mitego Afungukia Picha za ‘Pale Kati’ Zilizo Mdhalilisha Mwanamke, Azikana



Msanii Nay wa Mitego ambaye siku za karibuni wimbo wake mpya ‘Pale kati’ umefungiwa na Baraza la sanaa Taifa (BASATA) amefunguka na kusema kuwa suala la watu kusambaza picha kwenye mitandao ya jamii huku zikiwaonyesha wanawake wakiwa hawana nguo kabisa siyo kosa lake yeye kwani hakufanya hicho kitu bali kuna watu walitengeneza hizo picha wakiwa na malengo yao.

Nay wa Mitego amesema hayo katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kudai kuwa kuna watu walikuwa wanatengeneza picha hizo na kuzisambaza ila yeye hajafanya hivyo, na kudai kuwa alishajaribu kuwaripoti watu wengine ambao walikuwa wanafanya mchezo huo.

“Suala la picha za wimbo huo kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii huku zikionyesha wanawake wakiwa nusu uchi si suala langu mimi, maana dunia ya sasa kuna watu wanafanya ‘editing’ ya picha sana, kama mtakumbuka hata kipindi nimetoa ‘Shika adabu yako’watu walinitengeneza sana kwenye picha na kusambaza kwenye mitandao ya jamii, hivyo suala la picha hilo siyo tatizo langu” alisema Nay wa Mitego.

Mbali na hilo Nay wa Mitego amesema kuwa yeye hajaridhishwa na maamuzi ya BASATA kufungia wimbo wake mpya kwa kigezo cha picha kwani walipaswa kusubiri video itoke ndiyo inaeleza vizuri maana ya wimbo wake huo.

“Huwezi kufungia ‘Audio’ kwa sababu ya picha BASATA walitakiwa kusubiri nitoe video kwani video inatoa tafsiri nzuri ya wimbo huo na kama kungekuwa na tatizo kwenye video ndiyo tulipaswa kukaa na hawa walezi wetu katika muziki BASATA ili kuona tunaweza kurekebisha jambo gani katika video” alimalizia Nay wa Mitego

Powered By Blogger