Sunday, July 17, 2016

​Staa wa Pakistan auawa na kaka yake aliyechukia picha alizokuwa akiweka kwenye mitandao ya kijamii by fardyfadhil

Qandeel Baloch, aliyekuwa miongoni mwa mastaa wa mitandao ya kijamii nchini Pakistan, ameuawa na kaka yake katika mji wa Multan uliopo kwenye jimbo la Punjab. Alidai amemuua dada yake kwa heshima.


Polisi wamedai kuwa Baloch aliuawa na kaka yake kwenye nyumba ya familia yao baada ya kuchukizwa kwa muda mrefu na picha ambazo dada yake alikuwa akizipost mtandaoni.
Mwili wa mrembo huyo ukipelekwa kuzikwa
Hata hivyo kwa maisha ya Pakistan na sheria zake, Baloch alionekana kuwa ‘controversial’ japo alipendwa sana.
Alikuwa na karibu wafuasi 750,000 kwenye mtandao wa Facebook ambako video zake zilikuwa maarufu na kuzalisha mijadala nchini humo.
Alijipatia umaarufu zaidi nchini humo baada ya kuahidi kuwa angevua nguo online kama timu ya Pakistan ingeshinda kwenye mchezo wa  cricket dhidi ya mahasimu wao India.
Baloch alitengeneza pia vichwa vya habari baada ya kupost selfie kwenye Instagram akiwa na Mufti Abdul Qavi, moja ya viongozi wa dini nchini humo na kupelekea kusimamishwa wadhifa huo.
Kaka yake alidai kuwa skendo zake ndizo zilimfanya achukue uamuzi wa kumuua.

No comments:

Post a Comment

Powered By Blogger