
FA ameiambia Bongo5 kuwa nyimbo zake zote zimekuwa zikihitaji muda zaidi ya miezi mitatu kupotea kwenye masikio ya watu.
“Nilitamani niwe natoa ngoma kila miezi mitatu lakini inanishinda kwasababu pengine natengeneza muziki unakaa kwa muda mrefu,” amesema.
“Na pia naona kutaka kushindana ni kama kutaka kuprove kwamba mimi bado naweza, me I still got this na mimi sina kitu cha kuprove anymore. Najaribu kujipa nafasi, nifanye muziki kwa vile navyoona mimi inanifurahisha na naona hii ni sawa sawa kuliko kufuata trend kwamba ndio hivi wanavyofanya sasa hivi,” amesisitiza.
Wimbo wa mwisho kuufanya Mwana FA ni Asanteni Kwa Kuja.
No comments:
Post a Comment